visa vya ukweli
1) MAADILI
Allah Mwenye hikma Anasema: “Na hakika wewe una tabia tukufu.” (Suratul Qalam: 4) Mtukufu Mtume (saw) alisema: “Nimetumwa (kama mtume) ili kuja kukamilisha maadili.” (Jaame Al Saadaat, Juz, 1. Uk. 23) Maelezo mafupi: Kwa mwanadamu, maadili huleta heri na fahari katika ulimwengu huu na wepesi huko Akhera. Kunyanyua hadhi ya mtu katika ukaribu wake na Mwenyezi Mungu na humsaidia katika ukamilifu wa dini yake, Mitume wote, mawalii na wateule wa Mwenyezi Mungu walikuwa na maadili ya kupigiwa mfano, na kila mu’umini anapaswa kujipamba kwa maadili hayo, ili mizani ya amali iwe nzito zaidi Siku ya Hukumu. Mtukufu Mtume (saw) amesema: “Hatima ya muda wetu ni moja, kwa yule mwenye maadili mazuri. Maadili mabaya humfanya mtu ataabike kwa kubanwa mbavu kaburini na (adhabu ya) moto wa jahannam (huko akhera) na ukosefu wa marafiki katika ulimwengu huu.” Mtu hapaswi kupimwa kwa mujibu wa maarifa yake, utajiri au cheo, bali kwa mujibu wa tabia zenye kusifika, zinazomfanya akubalike mbele ya macho ya Allah na kwa kuwa mtukufu na msifiwa mbele ya macho ya watu. (Taz: Tadhkirah al-Haqaaiq, uk. 57)
1. Mtukufu Mtume (Saw) Na Nua’imaan
Nua’imaan Ibn Amr Ansaari alikuwa ni mmoja wa masahaba wa mwanzo wa Mtukufu Mtume (saw) na alikuwa na maumbile ya uchangamfu na ukarimu. Imesimuliwa kuwa siku moja Bedui mmoja aliwasili Madina na akampunzisha ngamia wake nyuma ya Msikiti (kisha) akaingia ndani ili awe kwenye hadhira ya Mtukufu Mtume (saw) Baadhi ya masahaba wa Mtume walimshawishi Nua’imaan kwa kusema “Ikiwa utamuua ngamia huyu, tutagawana nyama yake miongoni mwetu, na Mtukufu Mtume (saw) atalipa bei yake kwa mmiliki.” Kwa kufuata ushauri wao Nua’imaan alimuua mnyama yule. Mmiliki alipotoka nje ya msikiti na kukuta ngamia wake amekufa alikasirika sana na akaamua kulileta jambo hili mbele ya Mtukufu Mtume (saw). Nua’imaan wakati huo alikuwa amekwishakimbia. Mtukufu Mtume (saw) alitoka nje ya msikiti, akamuona ngamia aliyekufa na kuuliza “Ni nani anayewajibika kwa kitendo hiki? Wale waliokuwepo walimtuhumu Nua’imaan, hivyo Mtukufu Mtume (saw) akamtuma mtu kwenda kumleta Nua’imaan mbele yake. Habari zilivuma kuwa Nua’imaan alikuwa amejificha katika nyumba ya Dhubaa’h Bint Zubeir1 ambayo ilikuwa karibu na msikiti. Alikuwa ameingia kwenye shimo kisha akajifunika na majani mabichi. Mtukufu Mtume (saw) alielezwa juu ya maficho ya Nua’imaan na yeye na masahaba zake wakaelekea kwenye nyumba ya Dhubaa’h walipofika hapo, mjumbe aliomuonyesha Mtume (saw) maficho ya Nua’imaan ambaye Mtume (saw) alimuamuru (mjumbe) alifungue shimo. Baada ya kufanyika hilo, Nua’imaan aliibuka huku mashavu na kipaji chake cha uso vikiwa vimefunikwa na majani mabichi. Alipomuona, Mtukufu Mtume (saw) alimuuliza “Ewe Nua’imaan! Ni nini hiki ulichokifanya? Aljibu, “Ewe Mtume wa Allah (Naapa) kwa Allah! hao watu waliokuleta kwenye maficho yangu, ndio hao hao walionishawishi nimuue ngamia!” Mtukufu Mtume (saw) alitabasamu na kufuta majani kutoka kwenye mashavu na kipaji cha uso cha Nua’imaan kwa mikono yake mitakatifu. Kisha akalipa gharama ya ngamia kwa yule Bedui kwa niaba ya Nua’imaan
2. Khuzaima Na Mfalme Wa Urumi
Khuzaima Abrashi mfalme wa Arabuni, kamwe hakufanya kazi yoyote kubwa bila kwanza kutaka ushauri kutoka kwa mfalme wa Rumi ambaye alikuwa ni rafiki yake wa karibu. Wakati fulani, alikuwa na nia ya kupata maoni ya Mfalme (wa Urumi) juu ya heri ya wanawe, alimtumia barua kupitia mjumbe wake, katika barua aliandika: “Nahisi ninapaswa kutenga utajiri mkubwa kwa kila mwanangu wa kiume na wa kike ili wasije wakataabika baada yangu. Ni nini maoni yako juu ya jambo hili?” Mfalme wa Urumi Akajibu: “Utajiri ni kishawishi, hauna uaminifu na haudumu! Kitu bora kwa watoto wako itakuwa ni kuwapamba kwa maadili mema na tabia zenye kusifika, ambazo zitawapeleka kwenye uongozi wa kudumu katika ulimwengu huu na msamaha (wa dhambi) huko Akhera.
3. Mwendo Wa Imam Sajjad (As)
Wakati fulani, ndugu wa Imam Sajjad (as) alimuendea Imam (as) na akaan- za kumkashifu na kumtukana. Imam (as) hakutamka neno lolote kumjibu lakini, baada ya yule mtu kuondoka kwenye mkusanyiko ule, aliwageukia watu waliokuwepo na kusema: “Mmesikia aliyosema mtu huyu, sasa ninataka muambatane na mimi mkasikie kile nitakachosema kujibu kashfa na matusi yake” Masahaba wakakubali, “kwa hakika tutaambatana nawe, kwa kusema kweli tulitaraji kuwa ungemjibu wakati ule ule” Imam (as) aliondoka kuelekea kwenye nyumba ya mtu huyo na alisikika akisoma aya ya Qur’ani ifuatayo: وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ {134} “Na ambao wanazuia hasira (zao) na wanasamehe (makosa ya) watu; kwani Allah anawapenda wale wafanyao wema (kwa wengine) (Quran 3: 134) Msimuliaji anasema: “Tuliposikia kisomo cha aya hii, tulijua kwamba Imam (as) alikusudia kuonyesha wema kwa mtu ambaye punde tu alikuwa amemtukana” Alipofika kwenye nyumba ya mtu huyo, Imam (as) alimuita na akamjulisha kuwasili kwake. Alipomuona Imam, yule mtu akajua kuwa amekuja kujibu kashfa zake. Lakini, mara tu Imam (as) alipomuona yule mtu, alisema, “Ewe ndugu (yangu)! Ulikuja kwangu na kusema vitu vya kutisha na visivyopendeza. Ikiwa uliyoyasema juu yangu ni ya kweli, (basi) ninaomba msamaha kwa Allah, lakini ikwa sio, basi ninamuomba Allah ‘Azza wa Jallah akusame- he.” Yule mtu alishtushwa kusikia maneno haya na akatubu. Alimbusu Imam (as) baina ya macho na akaomba msamaha, akisema: “Matusi yangu na kashfa hayakuwa na msingi na hayawezi yakahusishwa na tabia yako. Kwa kweli matusi yale yananistahili mimi zaidi kuliko wewe.”
4. Ali (As) Na Mfanyabiashara Asiye Na Heshima
Imam Ali (as) wakati wa ukhalifa wake, mara nyingi alikuwa akitembelea masoko na kuwashauri na kuwaongoza wafanya biashara. Siku moja, alipokuwa akipita katika soko la tende, alimuona msichana mdogo akilia, Imam aliuliza sababu ya machozi yake ambapo (msichana) alieleza: “Bwana wangu alinipa dirham moja (kwa ajili) kununulia tende. Nilizinunua (tende) kwa mfanya biashara huyu, lakini niliporudi nyum- bani, bwana wangu alizikataa. Sasa ninataka kuzirudisha lakini mfanya biashara anakataa kuzichua.” Imam Ali (as) Ali alimgeukia mfanya biashara na kumuambia, “Mtoto huyu ni mtumwa na hana mamlaka yake mwenyewe. Chukua tende na umrudishie fedha yake.” Mfanya biashara alisogea mbele na huku wafanya biashara na watazamaji wengine wakimtazama, alimpiga Imam kifuani katika jitihada za kum- sukuma atoke mbele ya duka lake. Watu waliokuwa wakishuhudia tukio hilo, walikimbia na kumuambia huyo mwanaume: “Unafikiri unafanya nini? Huyu ni Ali Ibn Abi Talib (as)!” Uso wa mfanya biashara ulipauka alipokuwa amesimama akaduwaa. Mara moja alichukua tende kutoka kwa msichana na akamkabidhi fedha. Kisha akamgeukia Imam (as) akaomba, “Ewe Amirul Muuminuun! Niwie radhi na nisamehe.” Imam (as) alijibu,” Nitakuwa radhi na wewe tu pale utakapobadili tabia yako na kuwa njema na ukajali maadili na heshima.”
5. Maliki Ashtar
Wakati fulani, Maalik Ashtar alikwa akipita katika soko la Kufah akionekana masikini sana. Alikuwa amevaa nguo nzito (iliyotengenezwa kwa kitambaa cha turbai) na alikuwa ameweka turbai kichwani kwake badala ya kilemba. Mmoja wa wafanya biashara alikuwa amekaa dukani mwake macho yake yalipoangukia kwa Maalik. Alimtizama kwa twezo na kwa dharau akamtupia kipande cha udongo. Maalik alimpuuzia na aliendelea na safari yake. Hata hivyo mtu aliyem- tambua Maalik na aliyekuwa ameshuhudia tukio hilo, alimkanya mfanya biashara: “Aibu juu yako! Unamjua uliyemdhalilisha punde tu?” “Hapana.” Alijibu mfanya biashara “Alikuwa ni Maalik Ashtaar, sahaba wa Ali (as).” Baridi iliingia mwilini mwa mfanyabiashara alipowaza juu ya uovu alio- ufanya. Mara moja aliondoka na kumfuata Maalik ili akaombe msamaha. Alibaini kwamba Maalik alikuwa ameingia msikitini ambako alikuwa akisali na akamua kumsubiri. Maalik alipomaliza kusali tu yule mfanya biashara alimuangukia miguuni na kuanza kuibusu, Maalik alimnyanyua na kumuuliza alichokuwa akifanya. “Ninaomba msamaha kwa dhambi niliyofanaya,” alijibu mfanya biashara. Maalik akaeleza, “Hakuna dhambi juu yako. (Naapa) kwa Allah, nilikuja msikitini makhsusi kwa ajili ya kukuombea msamaha